Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele

Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hawafuatani na msafara katika safari, na ndani ya msafara kuna mbwa, au kengele inayotundikwa kwa wanyama ikitoa sauti mnyama anapotembea.

فوائد الحديث

Katazo la kufuga mbwa na kusuhubiana nao, isipokuwa mbwa wa kuwinda au wa ulinzi.

Malaika wanaojizuia kufuatana na msafara ni Malaika wa rehema, ama wale waandika matendo hao hawamwachi mtu akiwa nyumbani au safarini.

Katazo la kengele; kwani ni zumari katika mazumari ya shetani, na kuna kujifananisha na Wakristo.

Ni juu ya muislamu kujiweka mbali na yale yote yanayowaweka Malaika mbali naye .

التصنيفات

Malaika.