إعدادات العرض
Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa
Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."
[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî മലയാളം Português සිංහල دری Svenska አማርኛ অসমীয়া ไทย Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી Malagasy नेपाली Oromoo Română Nederlands Soomaali پښتو తెలుగు Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Српски Mooreالشرح
Maswahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi, waliona Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kupigana na maadui kuwa ni matendo bora, Basi Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akamuuliza Mtume Rehema na Amani zimshukie, je nao wapigane Jihadi? Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akawaelekeza kwenye Jihadi bora zaidi kwao, ambayo ni Hija iliyokubalika kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna, isiyo na dhambi na unafiki (Riyaa).فوائد الحديث
Jihadi ni katika amali bora kwa wanaume.
Haji kwa wanawake ni bora kuliko Jihadi, na ni miongoni mwa matendo bora kwao.
Amali zinazidiana ubora na zinatofautiana kulingana na mfanyaji.
Hija inaitwa Jihad; Kwa sababu ni Jihadi kwa ajili ya nafsi, na inahusisha kutoa mali na nguvu ya mwili, hivyo ni ibada ya mwili na mali kama kupigana Jihadi kwa ajili ya Allah.
التصنيفات
Fadhila za Hijjah na Umra.