إعدادات العرض
“Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu
“Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu
Kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepigana kwa kutaka kuonekana jasiri, na anayepigana kwa hamasa za ukabila, au anayepigana kwa kutaka kuonekana. Ni yupi kati ya hao anayepigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: “Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu."
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî മലയാളം සිංහල Русский دری Svenska አማርኛ অসমীয়া ไทย Tiếng Việt Кыргызча Yorùbá ગુજરાતી Malagasy नेपाली Oromoo Română Nederlands Soomaali پښتو తెలుగు Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Српски Wolof Mooreالشرح
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliulizwa kuhusu kutofautiana kwa malengo ya wapiganaji hao; mwenye kupigana kwa kutaka kuonekana jasiri, au kwa hamasa, au ionekane nafasi yake kati ya watu, au mengineyo, ni lipi kati ya haya lipo kwa ajili ya Allah? Akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu ni yule anayepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu.فوائد الحديث
Msingi katika kutengemaa kwa matendo na kuharibika kwake ni nia na kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Ikiwa lengo la Jihadi ni kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu, na likaunganishwa na lengo lingine la kisheria, kama vile kupata ngawira, basi haidhuru nia yake ya asili.
Kuwazuia maadui dhidi ya nchi na kulinda heshima za watu ni katika kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Fadhila ziliyotajwa kwa wapiganaji zinawahusu wale waliopigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe kuu.
التصنيفات
Adabu za Jihadi.