إعدادات العرض
Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala
Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî دری অসমীয়া ไทย አማርኛ Svenska Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી Malagasy नेपाली Oromoo Română മലയാളം Nederlands Soomaali پښتو తెలుగు Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Српски Mooreالشرح
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kuswali kunyoosha safu zao, na wasitanguliane wala wasirudi nyuma, na kwamba kuzinyoosha ni sehemu ya kukamilisha na ukamilifu wa Sala, na kuwa kupinda kwa safu ni dosari na ni upungufu ndani yake.فوائد الحديث
Sheria ya kuchunga kila kinachokamilisha swala na kuiweka mbali na upungufu.
Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kufundisha, kwani aliihusisha hukumu na sababu yake; ili iwe wazi hekima ya kuletwa sheria hiyo, na nafsi ipate hamasa ya kuitekeleza.