إعدادات العرض
Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake
Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake
Kutoka kwa Sahali bin Hunaif radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake"
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල አማርኛ অসমীয়া ગુજરાતી Tiếng Việt Nederlands پښتو नेपाली ไทย Svenska മലയാളം Кыргызча Română తెలుగు Malagasy ಕನ್ನಡ Српски ქართული Mooreالشرح
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeomba shahada na kuuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawa mkweli na mwenye ikhlasi katika nia yake hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu atamjaalia kupata daraja za mashahidi kwa nia yake ya kweli, hata akifa kitandani katika hali isiyokuwa jihadi.فوائد الحديث
Nia ya dhati na kufanya linalowezekana ni sababu ya kupata thawabu na malipo yaliyokusudiwa, hata kama amali inayotakiwa haijatekelezwa.
Himizo la jihadi na kuomba shahada katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa umma huu, kwani anaupa kupitia amali ndogo daraja za juu zaidi peponi.