Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao

Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao

Kutoka kwa Ally bin Abii Twaalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake Hariri kwa mkono wake wa kushoto, na dhahabu kwa mkono wake wa kulia, kisha akazinyanyua kwa mikono yake, akasema: "Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao".

[Ni sahihi kwa riwaya zake mbili] [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake nguo ya hariri au kipande chake, kwa mkono wake wa kushoto, na akachukua pambo la dhahabu au mfano wake kwa mkono wake wa kulia, kisha akasema: Hakika hariri na dhahabu ni haramu kuvivaa kwa wanaume, ama wanawake hivyo ni halali kwao.

فوائد الحديث

Amesema As- Sanadi: (Haram): Makusudio yake ni kuvitumia kwa kuvaa; na matumizi mengine ni ruhusa kwa wote, kama kubadilishana, kuvitoa sadaka na kuuza, na kutumia dhahabu kwa kufanya vyombo na kuvitumia ni haramu kwa wote.

Sheria ya Uislamu imepanua wigo kwa wanawake kwakuwa wao wanahitaji zaidi mapambo na mfano wake.

التصنيفات

Mavazi na Mapambo.