Dua ndio ibada

Dua ndio ibada

Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Dua ndio ibada", Kisha akasoma: "Na amesema Mola wenu Mlezi niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili" [Ghafir: 60].

[Sahihi]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dua ndio ibada, la msingi nikuwa yote iwe safi kwa ajili ya Allah, sawa sawa iwe ni kuomba jambo au kutaka jambo, kwa kumuuomba Allah Mtukufu ampe yenye manufaa kwake, na amkinge na yenye kumdhuru duniani na akhera, au dua ikiwa ni ibada, nayo ni kila anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika kauli na matendo ya wazi na ya siri, ibada za moyo au za mwili au za mali. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akatoa ushahidi juu ya hilo pale aliposema: Amesema Allah Mtukufu: "..Niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili"

فوائد الحديث

Dua ndio asili ya ibada na wala haifai kuilekeza kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Dua inaambatana na uhalisia wa kuabudu na kukiri utajiri wa Mola Mlezi na uwezo wake Yeye Mtukufu, na uhitaji wa mja kwake.

Kemeo kali likiwa ni malipo ya kiburi cha kutomuabudu Mwenyezi Mungu na kuacha kumuomba, nakwamba wale wanaofanya jeuri kumuomba Allah wataingia katika Jahannam wakiwa wanyonge madhalili.

التصنيفات

Fadhila za Dua.