إعدادات العرض
Alitufundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hotuba ya dharura (Haja)
Alitufundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hotuba ya dharura (Haja)
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alitufundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hotuba ya dharura (Haja)" Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, tunamtaka msaada na tunamuomba msamaha, na tunajilinda kwake kutokana na shari ya nafsi zetu, anaye muongoza Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na anayempoteza hakuna wa kumuongoa, na ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na nina shuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, "Enyi watu mcheni Mola wenu aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akaiumbia mke wake, na akatoa kutoka kwa wawili hao wanaume wengi na wanawake wengi, na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnaombana kwa jina lake nyinyi na familia zenu, hakika Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mchunga" [An-Nisaai:1] "Enyi mlio amini mcheni Mwenyezi Mungu ukweli wa kumcha, na wala msife ila mfe nanyi ni waislamu (wa kweli)" [Al-Imran: 102], "Enyi mlio amini mcheni Mwenyezi Mungu na mseme maneno ya sawa (70) Atakutengenezeeni mambo yenu na atakusameheni madhambi yenu, na atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume atakuwa amefaulu kufaulu kukubwa" [Al-Ahzaab: 70-71].
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو हिन्दी 中文 বাংলা Español Kurdî Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் සිංහල မြန်မာ ไทย 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە Hausa دری Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Kinyarwanda नेपाली Română Српски Soomaali Deutsch Moore Українська Български Tagalog Wolof Azərbaycan ქართული тоҷикӣ bm Македонскиالشرح
Anaeleza bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwafundisha hotuba ya haja (dharura), nayo ni ile inayosemwa wakati wa kufungua mazungumzo katika hotuba na wakati wa shida zao, kama hotuba ya ndoa na hotuba ya Ijumaa na nyinginezo, Na hotuba hii imekusanya maana tukufu, kwanzia kubainisha ustahiki wa Mwenyezi Mungu wa aina zote za kuhimidiwa, na kutaka msaada kutoka kwake yeye pekee asiye na mshirika wake, na stara ya madhambi na kusamehewa, na kuomba kinga kwake dhidi ya kila shari, na shari za nafsi na nyinginezo. Kisha akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa uongofu uko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, mwenye kumuongoza hakuna wa kumpoteza, na anayempoteza hana wa kumuongoza. Kisha akataja shahada ya tauhidi nakuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na shahada ya ujumbe kuwa Muhammadi ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ikahitimisha hotuba hii kwa aya hizi tatu zilizojaa amri ya kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, nakuwa malipo ya mwenye kufanya hivyo ni kutengemaa kwa matendo na kauli, na kusamehewa madhambi na kufutwa makosa na maisha mazuri duniani na kufaulu kwa kuipata pepo siku ya Kiyama.فوائد الحديث
Sunna ya kufungua hotuba ya ndoa na Ijumaa na zinginezo kwa hotuba hii.
Hotuba ni lazima ikusanye kuhimidi (kushukuru) na shahada mbili na baadhi ya aya ndani ya Qur'ani.
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwafundisha masahaba zake yale wanayoyahitaji katika dini yao.
التصنيفات
Hukumu na Masharti ya Ndoa.