Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam

Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto wa Duniani ni sehemu moja tu kutoka katika Moto wa Jahannam, Hivyo basi moto wa Akhera ukali wake unazidi Moto wa Duniani mara sitini na tisa, kila sehemu moja ya moto huo upo sawa na ukali wa moto wa Duniani. Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika Moto wa Duniani ulikuwa unatosha kuwaadhibu waliokuwamo humo, Akasema: Moto wa Jahannam umeuzidi moto wa Duniani kwa zaidi ya mara sitini na tisa, na mara zake zote hizo sitini na tisa ni sawa na mara moja kutokana na ukali wake.

فوائد الحديث

Kunatolewa tahadhari kutoka na Moto ili watu wajiepushe na matendo yatakayo wafikisha kwenye moto wa Jahannam.

Ukubwa wa Moto wa Jahannam na adhabu yake, na ukali wa joto lake.

التصنيفات

Kuamini siku ya mwisho, Sifa za pepo na moto.