إعدادات العرض
Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka
Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka
Kutoka kwa Abuu Muhammadi Al-Hasan bin Ally bin Abii Twalib mjukuu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na marashi yake (kipenzi chake), amesema: Nilihifadhi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka."
[Sahihi] [Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasaai]
الترجمة
العربية Español አማርኛ English اردو Indonesia বাংলা Français Türkçe Русский Bosanski සිංහල हिन्दी 中文 فارسی Tiếng Việt Tagalog Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் ไทย Deutsch پښتو অসমীয়া Shqip Nederlands ગુજરાતી Кыргызча नेपाली Lietuvių دری Српски тоҷикӣ Kinyarwanda Română Magyar Čeština Moore Malagasy Oromoo ಕನ್ನಡ Wolof Azərbaycan O‘zbek Українська ქართული Македонски ភាសាខ្មែរ ਪੰਜਾਬੀ मराठी Kirundi Kurmancî Bahasa Melayu မြန်မာالشرح
Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha lile linalokutia shaka ndani yake katika kauli na matendo kuwa limekatazwa au la, je ni halali au ni haramu, na ufanye yale usiyo na shaka nayo katika yale uliyo na uhakika na uzuri wake na uhalali wake.فوائد الحديث
Muislamu anatakiwa kujenga mambo yake juu ya yakini na kuacha yenye kutia shaka ndani yake, na awe na utambuzi katika dini yake.
Katazo la kutumbukia katika matamanio mabaya.
Ukitaka utulivu na raha achana na mambo yanayokutia shaka na kuyatupilia mbali.
Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, pale alipowaamrisha katika mambo ambayo ndani yake kuna raha ya moyo, na akawakataza katika yale yanayotia msongo na utata.
