Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu

Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anamtahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeyote atakayebeba silaha dhidi ya waislamu, kwa ajili ya kuwatisha au kuwapora, atakayefanya hivyo pasina haki, atakuwa ametenda kosa kubwa na dhambi miongoni mwa madhambi makubwa, na atakuwa kastahiki kemeo hili kali.

فوائد الحديث

Tahadhari kubwa ya waislamu kuwapiga ndugu zao waislamu.

Katika maovu makubwa na ufisadi mkubwa katika ardhi ni kutangaza silaha dhidi ya waislamu, na kufanya ufisadi kwa mauaji.

Kemeo lililotajwa halihusiani na kupigana kwa haki, kama kuwapiga waliokengeuka na mafisadi na wengineo.

Uharamu wa kuwatisha waislamu kwa silaha au kinginecho hata kama ni kwa sura ya mzaha.

التصنيفات

Uovu, Uovu, Adahabu ya Ujambazi., Adahabu ya Ujambazi.