إعدادات العرض
Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho
Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho
Kutoka kwa Abuu Umama amesema: Alinisimulia Amru bin Abasa radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français Tiếng Việt සිංහල Hausa Kurdî Português தமிழ் Русский አማርኛ অসমীয়া ગુજરાતી Nederlands پښتو नेपाली ไทย മലയാളം Svenska Кыргызча Română Malagasy ಕನ್ನಡ Српски తెలుగు ქართულიالشرح
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mola Mtukufu yu karibu zaidi na mja katika theluthi ya mwisho ya usiku, ikiwa utawezeshwa na ukaweza - Ewe Muumini - kuwa miongoni mwa wanaoabudu, na kuswali, na kumtaja Mwenyezi Mungu na kutubia wakati huu, basi ni jambo ambalo unapaswa kulishika na kujitahidi.فوائد الحديث
Muislamu anahimizwa kumtaja Mwenyezi Mungu mwisho wa usiku.
Nyakati zinazidiana ubora kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua na kuswali.
Amesema Muraik: Katika tofauti baina ya kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja,” na kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa mja na Mola wake Mlezi ni pale anapokuwa kasujudu”: Kinachokusudiwa hapa ni kuashiria wakati ambapo Mola anakuwa karibu zaidi na mja, yaani katikati ya usiku, na kinachokusudiwa hapo ni kueleza hali ya ukaribu wa mja na Mola ni pale anapokuwa katika hali ya kusujudu.
التصنيفات
Sababu za Kujibiwa Dua.