Mtu atakayepata furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Kiyama, ni yule atakayesema Laa ilaaha illa llah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), kwa kutakasa nia toka moyo mwake au nafsi yake

Mtu atakayepata furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Kiyama, ni yule atakayesema Laa ilaaha illa llah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), kwa kutakasa nia toka moyo mwake au nafsi yake

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Palisemwa ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni mtu gani atakayepata furaha zaidi ya uombezi wako siku ya Kiyama? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Nilijua kuwa ewe Abuu Huraira hatoniuliza mwingine hadithi hii kabla yako, kwa kile nilichokiona kwako, pupa yako juu ya hadithi, Mtu atakayepata furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Kiyama, ni yule atakayesema Laa ilaaha illa llah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), kwa kutakasa nia toka moyo mwake au nafsi yake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mtu mwenye furaha zaidi kuliko wote kwa uombezi wake siku ya Kiyama ni yule atakayesema: "Laa ilaaha illa llaah kwa kutakasa nia toka moyoni mwake" Yaani: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na asalimike na ushirikina na riyaa(kufanya mambo kwa kujionesha).

فوائد الحديث

Kuthibitisha uombezi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Akhera, nakuwa hautokuwa ila kwa watu wa tauhidi.

Uombezi wake -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kuomba kwake kupitia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yule atakaye stahiki Moto katika watu wa tauhidi ili asiuingie, na aliyeuingia atoke.

Ubora wa neno la tauhidi lililotakasiwa nia kwa ajili ya Allah Mtukufu na athari zake kubwa.

Kulihakikisha neno la tauhidi kunakuwa kwa kujua maana yake, na kufanyia kazi makusudio yake kwa namna inavyotakikana.

Ubora wa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na pupa yake juu ya elimu.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.