إعدادات العرض
Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda
Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda
Kutoka kwa Abul Abbasi Sahli bin Sa'di As-saai'diy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nijulishe amali ambayo nikiifanya atanipenda Mwenyezi Mungu na watu watanipenda, akasema: "Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහල دری অসমীয়া پښتو O‘zbek Tiếng Việt Македонски Nederlands ភាសាខ្មែរ ਪੰਜਾਬੀ తెలుగు ไทย Moore አማርኛ Magyar Azərbaycan ქართული ಕನ್ನಡ ગુજરાતી Українська Shqip Кыргызча Српски Kinyarwanda тоҷикӣ Wolof Čeština தமிழ் नेपाली മലയാളം kmr msالشرح
Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali ambayo akiifanya Mwenyezi Mungu atampenda na watu watampenda, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Atakupenda Mwenyezi Mungu utakapoacha yasiyo na msingi katika Dunia, na yale yasiyokunufaisha katika Akhera, na ukaacha yale yanayoweza kuwa na madhara katika dini yako, na watu watakupenda utakapoyapa nyongo yaliyoko mikononi mwao miongoni mwa vitu vya kidunia; kwa sababu wanayapenda kulingana na tabia zao za asili, na atakayebanana nao katika hayo watamchukia, na atakayewaachia watampenda.فوائد الحديث
Ubora wa kuipa nyongo dunia, nayo: Ni mtu kuacha yasiyofaa katika Akhera.
Kuipa nyongo dunia daraja yake ni kubwa kuliko unyenyekevu; kwa sababu unyenyekevu ni kuacha mambo ambayo huenda yakakudhuru, na kuipa nyongo dunia ni kuacha yasiyofaa katika Akhera.
Amesema Assanadi: Hakika Dunia inapendeka kwa watu, yeyote atakayepambana nao humo atachukiza kwao kwa kadiri ya hilo, na atakayewaacha na hicho wanachokipenda atapendeka ndani ya nyoyo zao kwa kiwango cha hilo.
