Kila wema ni sadaka

Kila wema ni sadaka

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kila wema ni sadaka"

[Sahihi]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa kila wema na kuwanufaisha wengine kuanzia kauli au matendo huwa ni sadaka, na kuna malipo na thawabu.

فوائد الحديث

Nikuwa sadaka haishii tu katika vile anavyovitoa mtu katika mali yake, bali inajumuisha kila kheri anayoifanya mwanadamu au kuitamka na kuifikisha kwa wengine.

Hapa kuna himizo la kutenda wema, na kila jambo lenye manufaa kwa wengine.

Kutodharau kitu katika wema, hata kama ni kidogo.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.