Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote

Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote

Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa nimepanda Punda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Punda akiitwa Ufairu, akasema Mtume: "Ewe Muadhi hivi unazijua haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na zipi haki za waja kwa Mwenyezi Mungu?" Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: " Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote" Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwanini nisiwape watu habari hii? Akasema Mtume: "Usiwape habari hii kwani watabweteka".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni kuwa wamuabudu yeye peke yake na wala wasimshirikishe yeye na kitu chochote. Na kuwa haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutowaadhibu wenye kumpwekesha ambao hawamshirikishi yeye na chochote. Kisha Muadhi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwa nini nisiwape watu habari hii njema ili wafurahi kwa jambo hili bora? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamkataza kwa kuogopea kuwa watategemea habari hiyo.

فوائد الحديث

Kumewekwa wazi haki za Mwenyezi Mungu ambazo amewajibisha kwa waja wake, nazo ni kumuabudu yeye, na wasimshirikishe na kitu chochote.

Kumewekwa wazi haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu ambayo ameiwajibisha yeye mwenyewe kwa fadhila zake na neema zake, na haki hiyo ni kuwaingiza peponi, na kutowaadhibu.

Katika hadithi hii kuna bishara njema na kubwa kwa wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, wale ambao hawamshirikishi Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu chochote, na kuwa mafikio yao ni kuingia peponi.

Alihadithia Muadhi hadithi hii kabla ya kufa kwake; kwa kuogopea kuingia kwenye madhambi ya kuficha elimu.

Kuna tahadhari ya kuacha kueneza baadhi ya hadithi kwa baadhi ya watu kwa kuogopea mtu kutofahamu maana yake; na hofu hiyo ni kwa yule ambaye hana matendo wala hayupo kwenye sheria miongoni mwa sheria.

Wafanyaji maasi wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wapo chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe, kisha mafikio yao yatakuwa peponi.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake., Ubora wa Tauhiid.