Hakitosimama Kiyama mpaka apite mtu juu ya kaburi la mtu aseme: Natamani ningekua nafasi yake

Hakitosimama Kiyama mpaka apite mtu juu ya kaburi la mtu aseme: Natamani ningekua nafasi yake

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka apite mtu juu ya kaburi la mtu aseme: Natamani ningekua nafasi yake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Kiyama hakitosimama mpaka mtu apite katika kaburi atamani laiti angelikuwa maiti mfano wake, na sababu ni kuihofia nafsi yake kwa kutoweka dini yake kwa kuzidiwa na batili na waovu, na kudhihiri kwa fitina na maasi na maovu.

فوائد الحديث

Kuna ishara ya kudhihiri maasi na fitina zama za mwisho.

Himizo la kuchukua tahadhari na kujiandaa na mauti kwa imani na matendo mema, na kujiweka mbali na mazingira ya fitina na balaa.

التصنيفات

Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa), Hali zawatu wema., Kuzitakasa Nafsi.