Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini

Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anatoa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu aliandika mambo yote ambayo yatatokea miongoni mwa mambo ya kuwakadiria viumbe kwa uchanganuzi kuanzia kuishi na kufa na riziki na mambo mengineyo aliyaandika katika Lauhil Mah-fuudh kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, na hayo aliyoyaandika hutokea kwa mujibu wa alivyopanga Hivyo basi kila kitu chenye kutokea, basi kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kukadiria kwake. Basi jambo lolote linalompata mja lisingeweza kumkosa, na lenye kumkosa lisingeweza kumpata.

فوائد الحديث

Ni wajibu kuamini hukumu na Kadari.

Na Kadari: Ni ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa kujua vitu vyote na kuviandika na kutaka kwake viwe na kuviumba.

Kuamini kuwa mipango ya Mwenyezi Mungu (Kadari) ilikwisha andikwa kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi kunaleta tija ya kuridhika na kujisalimisha na kukubali.

Kwa hakika Arshi ya Mwenyezi Mungu ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi.

التصنيفات

Ngazi za hukumu na Qadar.