إعدادات العرض
1- Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno: Muhifadhi Mwenyezi Mungu atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, utakapoomba basi muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu
2- Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini
3- Ametuhadithia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- naye ni mkweli mwenye kukubaliwa: "Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake kwenye tumbo la mama yake mchana arobaini na nyusiku arobaini
4- Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya