Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya

Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya

Imepokelewa kutoka kwa Twaausi kuwa yeye amesema: Niliwakuta watu miongoni mwa maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- wakisema kuwa kila kitu huwa kwa namna ilivyopangwa, akasema: Na nimemsikia Abdullah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake- anasema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila jambo linakuwa kwa mujibu wa lilivyopangwa; Mpaka kushindwa: Nako nikuacha jambo ambalo ni wajibu kulifanya au kulichelewesha katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hata kufanya jambo kwa ufanisi: Nako ni kufanya kwa uchangamfu na weledi katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu amepangilia jambo la kushindwa au kufanya kwa ufanisi na amepangilia kila kitu, hakuna chochote kinachotokea isipokuwa kinatokea kwa ujuzi wake Mwenyezi Mungu na kutaka kwake.

فوائد الحديث

Imewekwa wazi itikadi ya Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kuamini mipango ya Mwenyezi Mungu -Kadari-.

Kila kitu kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu mpaka kushindwa na kuweza kufanya jambo.

Uimara wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kupokea na kufikisha maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake.

Kuamini -Kadari- kheri zake na shari zake.

التصنيفات

Ni kuamini hukumu na mipangilio, Ngazi za hukumu na Qadar.