إعدادات العرض
Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla hajakaa
Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla hajakaa
Kutoka kwa Abuu Qatada As-sulami Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla hajakaa".
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda Українська नेपाली മലയാളം తెలుగు Bosanski Italiano ಕನ್ನಡ Kurdî Oromoo Română Soomaali Shqip Српски Wolof Tagalog Moore Malagasy தமிழ் Azərbaycan فارسی ქართული 中文 Magyarالشرح
Amemhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kuja msikitini na akaingia katika wakati wowote, na kwa lengo lolote, asali rakaa mbili kabla hajakaa, nazo ni rakaa mbili za salamu ya msikiti.فوائد الحديث
Sunna ya swala ya rakaa mbili kwa ajili ya salamu ya msikiti kabla ya kukaa.
Amri hii ni kwa atakayetaka kukaa, atakayeingia msikitini na akatoka kabla ya kukaa, amri hii haimuhusu.
Atakapoingia mwenye kuswali na watu wakiwa ndani ya swala, akaingia nao, basi hilo litamtosheleza na rakaa mbili.