Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba

Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba

Imepokewa kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba".

[Sahihi] [Imepokelewa na Addaar- Alqutni]

الشرح

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu atakapovaa khofu zake baada ya kutawadha, kisha akatengukwa udhu baada ya hapo, na akataka kutawadha, basi anatakiwa afute juu yake akitaka kufanya hivyo, na aswali nazo wala asizivue kwa muda maalum, isipokuwa atakapopatwa na janaba hapo atalazimika kuvua khofu na kuoga.

فوائد الحديث

Hairuhusiwi kufuta juu ya khofu mbili isipokuwa baada yakuwa na twahara kamili.

Muda wa kufuta kwa mkazi: Ni mchana na usiku (Masaa 24), na kwa msafiri: Ni michana mitatu na usiku wake (Masaa 72).

Kufuta juu ya Khofu mbili kunahusu tu hadathi ndogo nasi kubwa, ama hadathi kubwa haitakiwi kufuta, bali ni lazima kuvua khofu mbili na kuosha miguu miwili.

Ni sunna kuswali na viatu na khofu na mfano wake na hii ni kwa sababu ya kwenda kinyume na Mayahudi, na hii ni pale viatu vitakapokuwa twahara (visafi), na havina udhia kwa wenye kuswali, au msikiti, mfano kama miskiti iliyotandikwa mabusati mtu hatakiwi kuswali navyo.

Kufuta juu ya khofu mbili kuna urahisi na wepesi kwa umma huu.

التصنيفات

Kupaka juu ya Khofu mbili au soksi mbili