Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini

Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumjibu muadhini wakati wa kumsikia, na hii ni kwa sisi kusema mfano wa ayasemayo, sentensi kwa sentensi, Anaposema Allaahu Akbaru nasi tunasema Allaahu Akbaru, na anapotamka shahada mbili, nasi tunazitamka baada yake, Linaondolewa tamko la: (Hayya a'las swalaa, Hayya a'lal falaah) hapo tutasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah.

فوائد الحديث

Atamfuatisha muadhini wa kwanza baada ya kumaliza wa kwanza, hata kama waadhini watakuwa wengi; kwa sababu ya ujumla wa hadithi hii.

Atamjibu muadhini katika hali zake zote, ikiwa atakuwa hayuko chooni au akikidhi haja.

التصنيفات

Adhana na Iqama.