Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake

Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Imetoa faida hadithi ya Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa mwanadamu huwa katika tabia na mazoea ya rafiki yake na njia yake na mwenendo wake; kwaajili ya kuchukua tahadhari ya dini yake na tabia zake, achunguze na atazame ni nani anamfanya kuwa rafiki yake, anayemridhia dini yake na tabia zake basi anasuhubiana naye, na asiyemridhia anamuepuka, kwasababu tabia ni huiba (huiba toka kwa aliyekaribu) na ukaribu huathiri katika kuitengeneza hali au kuiharibu. La msingi nikuwa hadithi hii inaonyesha kuwa ni lazima kwa mtu aambatane na watu wa kheri; kwasababu ya kile kilichoko katika hilo miongoni mwa kheri.

التصنيفات

Hukumu za Kupenda na Kuchukia.