Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewakuta wazazi wake wawili wakati wa utuuzima, mmoja wao au wote wawili, na akawa hakuingia peponi

Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewakuta wazazi wake wawili wakati wa utuuzima, mmoja wao au wote wawili, na akawa hakuingia peponi

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewakuta wazazi wake wawili wakati wa utuuzima, mmoja wao au wote wawili, na akawa hakuingia peponi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba dua ya udhalili na fedheha mpaka akahisi kana kwamba mtu ametia pua yake kwenye mchanga – akarudia mara tatu – akaulizwa: Ni nani huyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, uliyemuombea dua mbaya? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayewakuta wazazi wake wawili, mmoja wao au wote wawili, wakati wa utuuzima, wakawa si sababu ya yeye kuingia Peponi; na hii ni kutokana na kukosa kuwatendea wema na kutowatii.

فوائد الحديث

Wajibu wa kuwatendea wema wazazi wawili nakuwa hilo ni moja ya sababu za kuingia Peponi, haswa wanapokuwa wazee na wanapodhoofika.

Kutowatii wazazi wawili ni katika madhambi makubwa.

التصنيفات

Ubora wa:Kuwatendea Wema wazazi wawili: