Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao

Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao, hivyo, nikiwakatazeni jambo basi liepukeni, na nikiwaamrisha jambo lifanyeni kadiri muwezavyo"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hukumu za kisheria zimegawanyika sehemu tatu: Zilizonyamaziwa, na makatazo, na maamrisho. Ama ya kwanza: Nayo ni ile ambayo sheria imeinyamazia: Kiasi kwamba hakuna hukumu, nakuwa asili ya mambo huwasiyo wajibu kuyafanya; Ama katika zama zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, ilikuwa ni lazima kujiepusha na kuuliza juu ya jambo ambalo halijatokea kwa kuhofia kuwekewa faradhi au katazo, kwani Mwenyezi Mungu aliliacha kwa ajili ya rehema kwa waja wake, na ama baada ya kufa kwake rehema na amani za Allah zimshukie, ikiwa swali liko katika mfumo wa fatwa au kujifunza kwa yale anayoyahitaji kuhusiana na mambo ya dini basi inajuzu bali imeamrishwa kufanya hivyo, na ikiwa ni katika namna ya jeuri na kuchimbua mambo, basi haya ndio maswali yanayokusudiwa kujiepusha nayo katika Hadithi hii. Na hii ni kwa sababu huenda ikapelekea katika yale yaliyowapata Wana wa Israeli, pale walipoamrishwa kuchinja ng'ombe yeyote lau wangelichinja ng'ombe yeyote basi wangelikuwa wametekeleza amri, lakini walitia mkazo, wakakaziwa pia. Ya pili: Ni makatazo; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyaacha, na anaadhibiwa mwenye kuyafanya, ni wajibu kuyaepeuka yote. Ya tatu: Ni maamrisho; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyafanya, na anaadhiwa mwenye kuyaacha, hivyo ni wajibu kuyafanya kwa kadiri ya uwezo.

فوائد الحديث

Tunapaswa kuzingatia kile ambacho ni muhimu zaidi na kinachohitajika, na kuacha kile kisichohitajika mara moja, na tusijishughulishe na kuuliza juu ya kile ambacho hakijatokea.

Ni haramu kuuliza maswali ambayo yanaweza kutatiza baadhi ya mambo, na kufungua mlango wa shaka ambayo husababisha kuhitilafiana kwingi.

Amri ya kuacha makatazo yote; Kwa sababu hakuna ugumu katika kuyaacha, na ndiyo maana katazo lilikuja kwa ujumla.

Amri ya kufanya kile kilichoamrishwa ni kwa kadiri ya uwezo; Kwa sababu mtu inaweza kuwa vigumu kwake kuitekeleza au akashindwa kuifanya; ndio maana amri ilikuja kuwa ifanyike kwa kadiri ya uwezo.

Katazo la kuuliza maswali mengi Wanachuoni wamegawanya kuuliza katika sehemu mbili: Moja wapo: Ni maswali yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza yale anayoyahitajia mtu kuhusiana na mambo ya dini, hili limeamrishwa, na miongoni mwa aina hii ni maswali ya Maswahaba, na aina ya pili: Ni maswali yanayokuwa katika sura ya kiburi na kujikalifisha, na hii ndiyo iliyoharamishwa.

Tahadhari kwa Umma huu dhidi ya kumpinga Nabii wake, kama ilivyotokea katika Umma zilizokuwa kabla yake.

Maswali mengi juu ya mambo yasiyohitajika na kutofautiana na mitume ni sababu ya maangamizo, na hasa katika mambo ambayo hayawezi kufikiwa, kama vile: Masuala ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeyajua, na hali za Siku ya Kiyama.

Katazo la kuuliza maswali katika mambo magumu, amesema Auzaai: Hakika Mwenyezi Mungu akitaka kumnyima mja wake baraka ya elimu, anaweka upotovu katika ulimi wake, na niliwaona watu wa namna hivyo kuwa ni watu wasio na elimu, na amesema bin Wahabi: Nilimsikia Maliki akisema: Mijadala tasa katika elimu hunaondoa nuru ya elimu katika moyo wa mtu.

التصنيفات

Manabii na Mitume waliotangulia - juu yao amani., Dalili za kimatamshi na namna ya kudadavua.