Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake

Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kuwaunga ndugu wa karibu kwa kuwatembelea na takrima za mwili na mali na mengineyo, nakuwa kufanya hilo ni sababu ya kukunjuliwa riziki, na kupewa umri mrefu.

فوائد الحديث

Ndugu wa karibu ni wale wa upande wa baba na mama, na kadiri anavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo anavyokuwa bora zaidi kwa kuungwa udugu.

Malipo huendana na matendo, atakayeunga udugu wake kwa wema na ihisani, naye pia Mwenyezi Mungu atamuunga katika umri wake na riziki yake.

Kuunga udugu ni sababu ya kukunjuliwa riziki na kupanuliwa kwake, na ni sababu ya umri mrefu, hata kama kifo na riziki vina muda maalum isipokuwa hili linaweza kuwa ni baraka katika riziki na umri, akafanya mengi katika umri wake na yenye manufaa zaidi kuliko atakavyofanya mwingine, na wanasema wanachuoni; ziada katika riziki na umri ni zaida ya uhalisia. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.