إعدادات العرض
Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume
Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português Русский Македонски नेपाली دری پښتو ગુજરાતી ភាសាខ្មែរ Shqip Українська Čeština Српски Kurdî ქართული Magyar ਪੰਜਾਬੀالشرح
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kusimamia ugawaji wa mirathi wazigawe kwa wastahiki wake kwa mgao wa uadilifu wa kisheria kama alivyotaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, ataanza kwa kuwapa wale wenye fungu lililokadiriwa tayari kisheria, kulingana na mafungu yao katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni: Theluthi mbili, na theluthi moja, na sudusu (moja ya sita) na nusu, na robo, thumunu (moja ya nane), mali itakayobakia baada ya hapo, hiyo atapewa ndugu wa karibu na maiti katika wanaume, na ndugu hao huitwa aswaba (warithi wasio na mipaka).فوائد الحديث
Hadithi hii ni kanuni katika ugawaji wa urithi.
Nikuwa ugawaji wa mirathi huanza na wale wanaostahiki kurithi waliopangiwa viwango.
Kuwa mali iliyobakia baada ya hao wenye kiwango cha kisheria ni ya ndugu wa mwanaume.
Kumtanguliza ndugu wa karibu kisha anayefuata, hatakiwi kurithi ndugu wa mbali kama baba mdogo, pamoja nakuwa ndugu wa karibu wapo kama baba.
Ndugu asiye na kiwango katika sheria hana haki ya kurithi endapo mali itamalizika, ikawa haikubakia chochote.
