Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote isipokuwa nimeyafanya, akasema: "Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah?

Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote isipokuwa nimeyafanya, akasema: "Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah?

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote isipokuwa nimeyafanya, akasema: "Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah?" Akarudia mara tatu. Akasema: Ndiyo, akasema: "Kwa hakika tamko hilo hufuta makosa hayo yote."

[Sahihi]

الشرح

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: @Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote madogo wala makubwa isipokuwa nimeyafanya, je mimi nitakuwa ni mwenye kusamehewa? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah? Akarudia kumwambia hivyo mara tatu, Basi akajibu: Ndiyo nashuhudia, Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa habari ya ubora na utukufu wa shahada mbili na namna inavyofuta makosa, na kuwa toba hufuta makosa yaliyopita.

فوائد الحديث

Utukufu wa shahada mbili na namna inavyoyashinda madhambi kwa yule atakayesema maneno hayo kwa dhati kutoka moyoni mwake.

Uislamu hufuta makosa yaliyopita huko nyuma.

Tauba ya kweli hufuta makosa yaliyopita huko nyuma.

Kurudia rudia katika kujifunza ni miongoni mwa miongozo ya bwana Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Utukufu wa shahada mbili, na kuwa shahada mbili ni sababu ya kuepuka kukaa Motoni milele.

التصنيفات

Ubora wa Tauhiid.