Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa

Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa swala tano za faradhi za usiku na mchana, na swala ya ijumaa kila wiki, na funga ya Ramadhani kila mwaka, vyote hivi hufuta madhambi madogo madogo yaliyo kati yake, kwa sharti la kuyaepuka madhambi makubwa, Ama madhambi makubwa kama zinaa na kunywa pombe haya hayafutwi isipokuwa kwa toba.

فوائد الحديث

Madhambi yako madogo madogo na yako makubwa.

Kufutiwa madhambi madogo madogo kumewekwa sharti la ya kuyaepuka makubwa.

Madhambi makubwa ni yale iliyokuja adhabu ndani yake katika dunia, au yaliyotajwa kuwa na ahadi ya adhabu huko Akhera; au Makasiriko, au kukawa na kemeo ndani yake, au kulaaniwa mfanyaji wake, kama zinaa na unywaji pombe.

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Ubora na fadhila za matendo mema., Ubora na fadhila za matendo mema., Fadhila za Swala., Fadhila za Swala.