Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi

Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amehimiza kufanya bidii katika kuswali Swala mbili za nyakati za baridi, ambazo ni sala ya Alfajiri na Alasiri, na akawabashiria kuwa mwenye kutekeleza haki zake kwa muda, na kwa jamaa na mambo mengine, basi zitakuwa ni sababu ya kuingia kwake Peponi.

فوائد الحديث

Fadhila ya kuhifadhi Sala ya Alfajiri na Alasiri; Kwa sababu Alfajiri ni wakati wa usingizi mzuri, na Alasiri ni wakati mtu anashughulika na kazi zake, basi atakayezihifadhi atakuwa na haki zaidi ya kuzihifadhi Swala zilizosalia.

Sala ya Alfajiri na Alasiri zimeitwa baridi mbili; Kwa sababu Swala ya Alfajiri ina ubaridi wa usiku, na Sala ya Alasiri ina ubaridi wa mchana, hata ikiwa ni katika wakati wa joto, ni nyepesi kuliko wakati wa kabla yake, au zimeitwa hivyo kwa kuzingatia kawaida ya nyakati nyingi huwa hivyo, kama ambavyo husemwa: Miezi miwili, kwa kumaanisha jua na mwezi.

التصنيفات

Fadhila za Swala.