Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi…

Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake

Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'di Karibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake".

[Sahihi]

الشرح

Anatuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika msingi miongoni mwa misingi ya tiba, nayo ni kinga ambayo mtu analinda kwayo afya yake, ambayo ni kupunguza kula, bali ale kwa kiasi cha kuziba tumbo lake na kupata nguvu ya kufanya kazi zake za lazima, na hakika chombo cha shari zaidi kilichowahi kujazwa ni tumbo, na hii ni kwa sababu ya matokeo ya shibe, kama maradhi mabaya yasiyohesabika yanayokuja haraka au kwa baadaye, ya siri au ya wazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ikiwa mtu hana namna zaidi ya kushiba, basi afanye kula kuwe kwa kiasi cha theluthi, na theluthi nyingine ya kinywaji, na theluthi nyingine ya pumzi ili asipate dhiki na madhara, na uvivu wa kutekeleza aliyomuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yake katika swala la dini yake au dunia yake.

فوائد الحديث

Kutozidisha katika kula na kunywa, na huu ni msingi unaokusanya misingi yote ya tiba, kwa kuwa katika kuzidisha kula kuna maradhi na magonjwa.

Lengo la kula, ni kuhifadhi afya na nguvu ambayo ndio usalama wa maisha.

Kujaza tumbo kwa chakula kuna madhara ya mwili na ya dini, amesema Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Tahadharini na kuvimbewa, kwani ni madhara kwa mwili na hutia uvivu wa kuswali".

Kula kwa mujibu wa hukumu kuna gawanyika: 1- Wajibu: Nako ni kule kunakohifadhi uhai na kuacha kwake kunaweza kupelekea madhara. 2- Inafaa: Nako ni kule kunakozidi katika kiwango cha wajibu na wala hakuna madhara kama ataacha. 3- Inachukiza: Nako ni kule kunakohofiwa madhara. 4- Haramu: Nako ni kule kunakojulikana kuwa kuna madhara. 5- Inapendeza: Nako ni kule kunakoweza kuwa msaada wa kufanya ibada na kumtii Mwenyezi Mungu, na imekusanywa vizuri katika hadithi katika daraja tatu: Ya kwanza: Kujaza tumbo. Ya pili: Matonge kadhaa yanayoweza kumpa nguvu ya kusimama. Ya tatu: Kauli yake: "Theluthi moja iwe kwa ajili ya chakula chake na theluthi nyingine kwa ajili ya kinywaji chake na theluthi nyingine kwa ajili ya pumzi yake" Na hii yote ikiwa kama aina ya chakula ni cha halali.

Hadithi hii ni kanuni miongoni mwa kanuni za tiba, kiasi ambacho hata elimu ya udaktari inazunguka katika misingi mitatu: Kuhifadhi nguvu, na kuilinda, na kuacha nafasi ya kupumua, hadithi imekusanya mambo mawili ya mwanzo katika hayo, kama ilivyokuja katika kauli yake Mtukufu: "Na kuleni na mnywe wala msifanye fujo kwani hakika Yeye hawapendi wafanyao fujo" [Al-Araf: 31].

Ukamilifu wa sheria hii, kiasi ambacho imekusanya masilahi yote ya mwanadamu katika dini yake na dunia yake.

Miongoni mwa elimu za sheria ni misingi ya udaktari na aina zake, kama ilivyokuja katika Asali na Habbati Saudaa.

Hukumu za sheria kujawa na hekima, na kwamba zimejengeka katika kuzuia madhara na kuleta manufaa.

التصنيفات

Kuyasema vibaya matamanio ya nafsi na ya kimwili.