Atakayemuua aliyechukua ahadi ya kulindwa, hatonusa harufu ya pepo, na hakika hurufu yake hupatikana kuanzia mwendo wa miaka arobaini

Atakayemuua aliyechukua ahadi ya kulindwa, hatonusa harufu ya pepo, na hakika hurufu yake hupatikana kuanzia mwendo wa miaka arobaini

Imepokewa Kutoka kwa Abdillah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Atakayemuua aliyechukua ahadi ya kulindwa, hatonusa harufu ya pepo, na hakika hurufu yake hupatikana kuanzia mwendo wa miaka arobaini".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari kubwa kwa atakayemuuwa aliyechukua ahadi ya kulindwa -Naye ni kafiri aliyeingia katika mji wa kiislamu kwa ahadi na amani- kuwa hatonusa harufu ya Pepo, na hakika harufu yake huwa kuanzia umbali wa mwendo wa miaka arobaini.

فوائد الحديث

Uharamu wa kumuua aliyechukua ahadi ya amani na kafiri anayeishi na waislamu, na aliyeomba amani katika makafiri, nakuwa jambo hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.

Aliyechukua ahadi: Ni kafiri aliyechukua ahadi ya kutowapiga vita waislamu na huku akiishi katika mji wake, na wao wasimpige vita, na dhimi: Ni yule anayeishi mji wa waislamu na akalipa jizia (kodi ya kichwa), na muomba amani: Ni mtu aliyeingia mji wa waislamu kwa mkataba na amani kwa muda maalumu.

Tahadhari ya kufanya hiyana katika makubaliano na wasiokuwa waislamu.

التصنيفات

Hukumu za waliokuwa kwenye Dhimma- Mkataba-