Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera

Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera Ama kafiri hulishwa kwa mema aliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, mpaka akifika Akhera anakuwa hana jema lolote ambalo atalipwa nalo."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waumini, na uadilifu wake kwa makafiri. Ama muumini hazipungui thawabu za mema aliyoyafanya; Bali hulipwa hapa duniani wema kwa utiifu wake, pamoja na kulimbikiziwa malipo yake huko Akhera; Na huenda akahifadhiwa malipo yake yote huko Akhera. Ama kafiri, Mwenyezi Mungu humlipa malipo kutokana na wema alioufanya kwa malipo ya mambo yaliyo mazuri hapa Duniani, mpaka inakuwa akifika Akhera, anakuwa hana thawabu na malipo atakayo lipwa huko, kwa sababu matendo mema ambayo yatamfaa hapa Duniani na Akhera lazima awe mtendaji wake ni muumini.

فوائد الحديث

Nikuwa yeyote atakaye kufa hali ya kuwa ni kafiri basi matendo yake hayatomfaa.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Maisha ya Akhera., Uislamu