إعدادات العرض
Haifai kujidhuru wala kumdhuru mwingine
Haifai kujidhuru wala kumdhuru mwingine
Kutoka kwa Abuu Saidi Sa'di bin Maaliki bin SInani Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haifai kujidhuru wala kumdhuru mwingine."
[Ni nzuri (Hasan)] [Imepokelewa na Ibnu Maajah, Daaruqutni na wengineo huku inafika kwa Mtume]
الترجمة
العربية Español አማርኛ English اردو Indonesia বাংলা Français Türkçe Русский Bosanski සිංහල हिन्दी 中文 فارسی Tiếng Việt Tagalog Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ ไทย Deutsch پښتو অসমীয়া Shqip Nederlands ગુજરાતી Кыргызча नेपाली Lietuvių دری Српски тоҷикӣ Kinyarwanda Magyar Čeština Moore Malagasy Oromoo ಕನ್ನಡ Wolof Azərbaycan O‘zbek Українська ქართული Македонски ភាសាខ្មែរ Bambara ਪੰਜਾਬੀ मराठी Kirundi Kurmancî Bahasa Melayuالشرح
Amebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine, ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka.فوائد الحديث
Katazo la kulipiza kwa zaidi ya vile ulivyofanyiwa.
Mwenyezi Mungu hakuwaamrisha waja wake lolote lenye kuwadhuru.
Hadithi ni kanuni katika kuharamisha kujidhuru, na kudhuru kwa kauli au vitendo au kuacha.
Katika kanuni za sheria: Ni "Madhara huondoshwa", Hivyo, sheria haikubaliani na madhara, na inakataza kujidhuru.
