إعدادات العرض
Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani
Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani
Imepokewa Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Tiếng Việt ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or नेपाली Malagasy Kinyarwanda తెలుగు Lietuvių Oromoo Română മലയാളം Nederlands Soomaali Српски Українська Deutsch ಕನ್ನಡالشرح
Amekataza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa muislamu kusema katika maneno yake: "Akitaka Mwenyezi Mungu na akitaka fulani", Au akitaka Mwenyezi Mungu na fulani; Na hii ni kwa sababu matashi ya Mwenyezi Mungu na maamuzi yake ni ya moja kwa moja na hakuna yeyote anaye shirikiana naye, Na katika matumizi ya kiunganishi "Na" hii inamaanisha kuwa kuna mtu anayeshirikiana pamoja na Mwenyezi Mungu na kuwa wako sawa katika maamuzi. Lakini aseme: Akitaka Mwenyezi Mungu, kisha fulani, Hivyo basi afanye matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: " Kisha" badala ya "Na", kwa sababu kiunganishi "Kisha" humaanisha kuja baada ya kitu kingine na kuchelewa pia.فوائد الحديث
Uharamu wa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka", na mfano wa matamshi kama haya ambayo yatamaanisha kuunganisha neno na Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "Na"; kwa sababu hii ni katika shirki ya matamshi.
Inafaa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka", na mfano wa hayo ambayo yanamaanisha kuunganisha maneno kwa kiunganishi "Kisha"; kwa kuwa hakuna katazo ndani yake.
Hapa kumethibitishwa matashi kwa Mwenyezi Mungu, na matashi ya mja, nakuwa matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Katazo la kuwashirikisha viumbe katika matashi ya Mwenyezi Mungu hata kama ni kwa matamshi.
Ikiwa mtu ataitakidi kuwa matashi ya mja ni sawa na matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuenea kwake na kutokuwa na mipaka, nakuwa mja ana matashi binafsi ya kwake mwenyewe, hii ni shirki kubwa, ama akiitakidi kuwa matashi ya mja yanakaribia matashi ya Mwenyezi Mungu; hii ni shirki ndogo.