Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni

Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni

Imepokelewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuifikisha elimu kutoka kwake katika Qur'ani na mafundisho yake (Sunna), hata kama kitu kitakuwa kidogo kama aya moja toka ndani ya Qur'ani au hadithi, kwa sharti mfikishaji awe mjuzi katika kile anachokifikisha na kuwalingania watu kwacho. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna ubaya kusimulia kuhusu wana wa Israeli kwa yale yaliyotokea kwao katika matukio, yale yasiyokinzana na sheria yetu. Kisha akatahadharisha kumzulia uongo, nakuwa yeyote mwenye kumzulia uongo kwa makusudi basi ajiandalie mwenyewe makazi yake motoni.

فوائد الحديث

Himizo la kufikisha sheria ya Allah, nakuwa mtu anajukumu la kuyafikisha aliyoyahifadhi na kuyaelewa hata kama ni kidogo.

Ulazima wa kutafuta elimu ya kisheria, ili mtu awe na uwezo wa kumuabudu Allah na kuifikisha sheria yake kwa sura sahihi.

Uwajibu wa kuhakiki usahihi wa kila hadithi kabla ya kuifikisha au kuisambaza kwa kutahadhari kutoingia katika ahadi hii ya adhabu kali.

Himizo la ukweli katika maneno, na kuchukua tahadhari katika mazungumzo, ili mtu asiingie katika uongo, na hasa hasa katika sheria ya Allah -Aliyetakasika na kutukuka-.

التصنيفات

Umuhimu wa sunnah naNafasi yake., Hukumu ya Kulingania na kuelekeza kwa Mungu.