إعدادات العرض
Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo
Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo
Kutoka kwa Salim bin Abil Ja'di amesema: Mtu mmoja alisema: Laiti ningeswali nikastarehe, wakawa kana kwamba wamelitia dosari hilo, akasema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo".
[Sahihi] [Imepokelewa na Abuu Daud]
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda नेपाली മലയാളം తెలుగు Bosanski Italiano ಕನ್ನಡ Kurdî Oromoo Română Soomaali Shqip Српски Українська Wolof Tagalog Moore Malagasy தமிழ் Azərbaycan فارسی ქართული 中文 Magyarالشرح
Akasema mtu mmoja katika Masahaba: Laiti ningeliswali nikastarehe, waliokuwa naye waka kana kwamba wamemuabisha kwa hilo, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Ewe Bilali! Nyanyua adhana na simamisha swala; ilitustarehe kwayo; na hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na raha ya roho na moyo.فوائد الحديث
Raha ya moyo iko ndani ya swala; kwani ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kemeo kwa mvivu katika ibada.
Atakayetekeleza wajibu ulio juu yake, na akajiweka mbali na dhima, atapata raha kwa ibada hiyo na atahisi utulivu.