إعدادات العرض
Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo
Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muhammadi Abdallahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo".
[Amesema Nawawi: Hadithi hii ni sahihi] [Imepokelewa na katika kitabu cha Al-Hujjah kwa msururu sahihi wa wasimulizi]
الترجمة
العربية Español አማርኛ English اردو Indonesia বাংলা Français Türkçe Русский Bosanski සිංහල हिन्दी 中文 فارسی Tiếng Việt Tagalog Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ ไทย Deutsch پښتو অসমীয়া Shqip Nederlands ગુજરાતી Кыргызча नेपाली Lietuvių دری Српски тоҷикӣ Kinyarwanda Magyar Čeština Moore Malagasy Oromoo ಕನ್ನಡ Wolof Azərbaycan O‘zbek Українська ქართული Македонски ភាសាខ្មែរ Bambara ਪੰਜਾਬੀ मराठी Kirundi Kurmancî Bahasa Melayuالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanadam hawezi kuwa muumini mwenye imani kamili ya wajibu mpaka mapenzi yake yafuate yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa amri na makatazo na mengineyo, ayapende aliyoamrishwa, na ayachukie aliyokatazwa.فوائد الحديث
Hadithi hii ni kanuni ya kujisalimisha katika sheria na kutii.
Tahadhari kwa mwanadamu kuwa yeyote mwenye kuipa kipaumbele akili au mazoea na akaitanguliza kuliko yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi huyu imani kwake imekanushwa.
Ulazima wa kuifanya sheria kuwa ndio muamuzi katika kila kitu, kwa kauli yake: "Yale niliyokuja nayo".
Nikuwa imani inaongezeka kwa kumtii Mwenyezi Mungu na inapungua kwa kumuasi.
