إعدادات العرض
Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina
Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina
Kutoka kwa Ukba Bin Aamir Al Juhaniy -Radhi za Allah ziwe juu yake: Yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuja kwake kundi, akawaunga mkono watu tisa na akamuacha mmoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewaunga mkono watu tisa na ukamuacha huyu? akasema: "Huyo yuko na hirizi", akaingiza mkono wake akaikata, akamuunga mkono, akasema: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina"
[Ni nzuri] [Imepokelewa na Ahmad]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە Tiếng Việt پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or Malagasy Čeština नेपाली Oromoo Nederlands Soomaali తెలుగు ไทย Српски മലയാളം Kinyarwanda Română ಕನ್ನಡ Lietuvių Wolof Magyar ქართული Mooreالشرح
Walikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na idadi yao walikuwa kumi, akawaunga mkono tisa miongoni mwao juu ya Uislamu na kufuata sheria, na hakumuunga mkono wa kumi, alipoulizwa kuhusu sababu yake, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo kavaa hirizi, nayo ni kila kinachotundikwa, ikiwemo shanga na vinginevyo kwa lengo la kuzuia kijicho au madhara. Yule bwana akaingiza mkono wake mahali ilipo hirizi na akaikata na akaepukana nayo, hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuunga mkono, na akasema akitahadharisha kuhusu hirizi na akibainisha hukumu yake: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya shirki".فوائد الحديث
Atakayemtegemea asiyekuwa Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atampeleka kinyume na lengo lake.
Kuamini kuwa kutundika hirizi ni miongoni mwa sababu za kuzuia udhia wa kijicho, ni shirki ndogo, na ama akiitakidi kuwa inamnufaisha yenyewe, hii ni shirki kubwa.