إعدادات العرض
Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake
Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands සිංහල ไทย دری Akan Azərbaycan Български Fulfulde Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy नेपाली or Română Kinyarwanda тоҷикӣ O‘zbek Moore Wolof Oromoo Српски Soomaali bm Українська Tagalog rn km ქართული Македонскиالشرح
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye hiji kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na akawa hakufanya yasiyofaa; Na yasiyofaa hapa maana yake ni tendo la ndoa na vitangulizi vyake, kama busu, kugusana, neno hili hutumika pia kumaanisha maneno machafu, na akawa hakufanya uovu; kwa kufanya maasi na madhambi, Na miongoni mwa uovu ni kufanya makatazo ya ihiramu (Hija), atarudi kutoka katika hija yake akiwa kasamehewa, kama azaliwavyo mtoto akiwa amesalimika kutokana na madhambi.فوائد الحديث
Uwovu pamoja na kuwa umekatazwa katika hali zote, katazo hilo linatiwa mkazo katika Hija kwa kuheshimu na kutukuza ibada ya Hija.
Mwanadamu huzaliwa pasina kuwa na makosa akiwa kaepukana na madhambi; hivyo hawezi kubeba madhambi ya mwingine.
التصنيفات
Fadhila za Hijjah na Umra.