Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo

Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kubaki tupu bila ibada ya swala ndani yake, yakawa kama makaburi ambayo hayaswaliwi ndani yake, Na akakataza kurudi mara kwa mara kutembelea kaburi lake na kukusanyika hapo kwa namna ya mazoea; kwani hilo ni njia ya kuelekea katika ushirikina, Na akaamrisha kumtakia rehema na amani juu yake mahala popote katika uso wa ardhi; kwani dua hizo humfikia kutoka kwa aliyekaribu na aliyembali kwa kiwango sawa, haina haja ya kurudi mara kwa mara katika kaburi lake.

فوائد الحديث

Katazo la kuziacha nyumba bila ya kumuabudia Allah Mtukufu ndani ya majumba hayo.

Katazo la kufunga safari kwa ajili ya kuzuru kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwani yeye aliamrisha kumuombea rehema juu yake na akaeleza kuwa zinamfikia, bali hufungwa safari kwa kuukusudia msikiti pekee na kusali ndani yake.

Uharamu wa kulifanyia matembezi kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni sikukuu, kwa kukithirisha kulizuru kwa namna maalum na kwa nyakati maalum, na vile vile ziara ya kaburi lolote.

Utukufu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Mola wake, kwa kuwekwa sheria ya kumtakia rehema kwa kila zama na kila mahali.

Kiasi kwamba katazo la kuswali makaburini limepitishwa kwa maswahaba; kwa ajili hii alikataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kufanywa kuwa kama makaburi hakusaliwi ndani yake.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.