Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi

Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuendelea kubaki katika dhulma kwa kufanya maasi na ushirikina na kuwadhulumu watu haki zao, kwani Allah Mtukufu humpa muda dhalimu na humchelewesha na humpa umri mrefu na mali nyingi hamharakishii adhabu; ikiwa hatotubia basi humchukua mara moja na huwa hambakishi na huwa hamuachi kwa sababbu ya wingi wa dhulma zake. Kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika adhabu yake ni chungu na ni kali" [Hud:102]

فوائد الحديث

Kwa mwenye akili analazimika kufanya haraka kuomba toba, na asijiaminishe na adhabu za Mwenyezi Mungu andapo atakuwa katika dhulma.

Mwenyezi Mungu kuwapa muda madhalimu na kutokuwaharakishia adhabu huko ni kuwaleta taratibu na ni kuwaongezea adhabu endapo hawatotubia.

Dhulma ni katika sababu za Mwenyezi Mungu kuziangamiza umma.

Anapouangamiza Mwenyezi Mungu mji huenda kukawa na watu wema ndani yake, hawa watafufuliwa siku ya Kiyama katika matendo mazuri waliokufa nayo, na haidhuru wao kukumbwa na adhabu.

التصنيفات

Akida- Itikadi-, Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Tabia mbovu.