Atakayeacha swala ya Lasiri basi yameporomoka matendo yake

Atakayeacha swala ya Lasiri basi yameporomoka matendo yake

Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa amesema: Iswalini mapema swala ya Lasiri, kwani Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeacha swala ya Lasiri basi yameporomoka matendo yake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuchelewesha swala ya Lasiri nje ya wakati wake kwa makusudi, nakuwa mwenye kufanya hivyo yatakuwa yamebatilika matendo yake na yameharibika matendo yake na yameenda patupu.

فوائد الحديث

Himizo la kuihifadhi swala ya Lasiri mwanzo wa wakati wake na kuiharakisha.

Ahadi ya dhabu kali kwa atakayeiacha swala ya Lasiri ambayo ni swala ya kati kati, na kuitoa nje ya wakati wake maalum kwa amri iliyokuja katika kauli yake Mtukufu: "Zihifadhini swala na swala ya kati kati" [Al-Baqara: 238].

التصنيفات

Wajibu wa Swala na Hukumu ya Mwenye kuiwacha.