Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza

Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto umezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo nafsi inayatamani, kama kufanya maharamisho au uzembe katika mambo ya wajibu; Atakayeendekeza matamanio ya nafsi yake katika hilo atastahiki moto, nakuwa Pepo imezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo yanachukiwa na nafsi; kama kudumu katika maamrisho na kuacha maharamisho na kuvumilia juu ya hilo, atakapovumilia na akapigana vita na nafsi yake juu ya hilo atastahiki kuingia Peponi.

فوائد الحديث

Miongoni mwa sababu za kuingia katika matamanio ni shetani kuyapamba maovu na machafu, mpaka nafsi inayaona kuwa ni mazuri na kisha kuyaelekea.

Amri ya kujitenga mbali na matamanio yaliyoharamishwa; kwa sababu hayo ni njia ya kuelekea motoni, na kuvumilia juu ya kero; kwani ni njia ya kuelekea Peponi.

Ubora na fadhila za kupigana na nafsi na kuwa na bidii katika ibada na kuvumilia kero na tabu zinazo zizunguka ibada.

التصنيفات

Sifa za pepo na moto.