Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha

Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha

Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Jibrili akikariri kwake na akimuamrisha kumjali jirani, ambaye ni wakaribu kimakazi, sawa awe muislamu au kafiri, na sawa sawa awe ndugu wa karibu wa mbali, kwa kuhifadhi haki zake na kutomuudhi, na kumtendea wema na kuvumulia kero zake, mpaka akadhania -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kule kuitukuza kwake haki ya jirani na kitendo cha Jibrili kulirudiarudia hilo kwamba utakuja kuteremsha wahyi wa kumpa katika mali zake jirani yake atakayebakia baada ya kifo chake.

فوائد الحديث

Ukubwa wa haki za jirani na uwajibu wa kulichunga hilo.

Msisitizo juu ya haki za jirani kwa kutoa usia, hii inamaanisha ulazima wa kumkirimu na kujipendekeza kwake na kumtendea wema, na kumzuilia madhara, na kumtembelea wakati wa maradhi, na kumpongeza wakati wa furaha, na kumpa pole wakati wa msiba.

Kila unavyozidi kuwa karibu mlango wa jirani ndivyo ambavyo haki yake inazidi kuwa na mkazo zaidi.

Ukamilifu wa sheria katika yale iliyokuja nayo, katika yale yenye kuitengeneza jamii kama kumtendea wema jirani, na kumzuilia madhara.

التصنيفات

Suluhisho na hukumu za ujirani.