Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu

Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu

Kutoka kwa Ubaadah bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu, na tusiwanyang'anye uongozi wanaostahiki, na tusema ukweli mahala popote tuwapo, tusiogope kwa Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumu.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alichukua ahadi na mkataba kutoka kwa Masahaba ya utii kwa wenye mamlaka na watawala katika wepesi na ugumu, na katika hali ya utajiri na umasikini, na sawa sawa amri zao ziwe katika yale wanayoyapenda au kuyachukia, hata kama watawala watajipendelea kuliko raia kwa mali ya umma au vyeo au mengineyo, basi ni wajibu kwao kusikiliza na kutii katika wema, na wasitoke dhidi yao, kwa sababu fitina na ufisadi katika kupigana nao ni mambo makubwa na ni mabaya mno kuliko ufisadi unaotokea kwa sababu ya dhulma zao, na katika mambo waliyoyachukulia kiapo ni waseme kweli mahali popote, wakilitakasa hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hawamuogopi mwenye kuwalaumu.

فوائد الحديث

Matunda ya kusikia na kuwatii viongozi ni kukusanyika kwa nguvu na umoja wa waislamu na kuacha migawanyiko.

Uwajibu wa kusikia na kuwatii wenye mamlaka katika yale yasiyomuasi Mwenyezi Mungu katika hali ya wepesi na uzito, na katika mambo yenye kufurahisha na kuchukiza na kule kujipendelea wanakojipendelea wao.

Uwajibu wa kusema kweli mahala popote tuwapo, bila kuogopa katika jambo la Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulauma.

التصنيفات

Siasa ya Kisheria., Kutoka kwa ajili ya kumpinga kiongozi.