إعدادات العرض
Msichupe mipaka katika kunisifu, kama walivyochupa mipaka Wakristo kwa mwana wa Mariam; Bila shaka, mimi ni mja wake, na semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake
Msichupe mipaka katika kunisifu, kama walivyochupa mipaka Wakristo kwa mwana wa Mariam; Bila shaka, mimi ni mja wake, na semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake
Imepokelewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Msichupe mipaka katika kunisifu, kama walivyochupa mipaka Wakristo kwa mwana wa Mariam; Bila shaka, mimi ni mja wake, na semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் සිංහල မြန်မာ Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە Hausa ไทย دری Български Fulfulde Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy or Română Kinyarwanda тоҷикӣ O‘zbek Akan नेपाली Moore Azərbaycan Wolof Oromoo Soomaali Українська bm km rn ქართული mkالشرح
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupitiliza na kuvuka mpaka wa kisheria katika kumsifu, na kumsifu kwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu na matendo yake ambayo ni yake pekee, au kusema kuwa anajua mambo yaliyo jificha, au anastahiki kuombwa pamoja na Mwenyezi Mungu, kama walivyofanya Wakristo kwa Issa mwana wa Mariam -Amani iwe juu yake- Kisha akaweka wazi kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu, na akaamrisha tuseme kuhusu yeye: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake.فوائد الحديث
Tahadhari ya kuvuka mpaka wa kisheria katika kuzikuza sifa; kwani hilo hupelekea katika ushirikina.
Aliyoyatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tayari yamekwisha tokea katika umma huu, kundi likachupa mipaka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kundi kwa watu wa nyumba yake, na kundi kwa mawalii wake (wacha Mungu), wakatumbukia katika ushirikina.
Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye ni mja anaelelewa na Mwenyezi Mungu haifai kuelekezewa chochote katika mambo mahususi ya kiuungu.
Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye katumwa kutoka kwa Allah hivyo, ni wajibu kumsadikisha na kumfuata.