Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni

Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni

Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika Pepo hata kama ataadhibiwa kwa baadhi ya madhambi yake, nakuwa atakayekufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote atabakizwa milele Motoni.

فوائد الحديث

Ubora wa tauhidi, nakuwa ni sababu ya kuokoka na kukaa milele Motoni.

Ukaribu wa Pepo na Moto kwa mja nakuwa hakuna baina yake na hivyo viwili isipokuwa kifo.

Tahadhari inatolewa ya kujiepusha na ushirikina mdogo au mkubwa, kwa sababu kuokoka na moto ni kwa kuuepuka.

Mazingatio katika matendo huangaliwa mwisho wake.

التصنيفات

Ushirikina., Sifa za pepo na moto.