Atakaye jifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao

Atakaye jifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao

Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye jifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao".

[Ni nzuri]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye jifananisha na watu fulani katika makafiri au waovu au wema -na hii ni pale atakapofanya jambo katika mambo yao mahususi, kama itikadi au ibada au tamaduni basi naye ni miongoni mwao-; kwa sababu kujifananisha nao katika muonekano kunapelekea kujifananisha nao kiundani, na hakuna shaka kuwa kujifananisha na watu fulani kunasababishwa na kupendezwa nao, na huenda kukapelekea kuwapenda na kuwatukuza na kuwategemea, na hili huenda likampelekea mtu hata kujifananisha kiundani na katika ibada -Tunamuomba Allah atukinge na hilo-.

فوائد الحديث

Tahadhari ya kujifananisha na makafiri na waovu.

Himizo la kujifananisha na watu wema na kuiga kutoka kwao.

Kujifananisha katika muonekano hutia mapenzi katika moyo.

Mtu hupata kemeo la adhabu na madhambi kulingana na namna ya kujifananisha na aina yake.

Katazo la kujifananisha na makafiri katika dini yao na katika desturi zao mahususi kwao, ama yasiyokuwa hayo kama kujifunza ufundi na mfano wake hayaingii katika katazo.

التصنيفات

Kujifananisha kulikokatazwa